- Kiongozi wa muungano wa NASA amesema kuwa mabalozi wa nchi za Magharibi wanafanya kosa kubwa kwa kuungana na Jubilee kuukandamiza upinzani
- Katika mahojiano, Raila alisema kuwa msukumo anaopata kutoka kwa mabalozi wa kimataifa sio wa kulisaidia taifa hili la Kenya
- Alisisitiza kuwa mabalozi hao wanataka kujinufaisha tu kibiashara kupitia kwa serikali
Kiongozi wa mrengo wa upinzani, Raila Odinga amesema kuwa mabalozi wa nchi za kimataifa hawana lolote la kuwasaidia Wakenya ila tu kuungana na serikali kujinufaisha kibiashara.
Raila alionekana kutemwa na mabalozi kadha wa kimataifa walioonekana kumuunga mkono Uhuru Kenyatta na kupuuzilia mbali tetesi za Raila kuwa haki ni lazima itendeke.
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Habari Nyingine: Pata kufahamu mali inayomilikiwa na familia za Raila Odinga na Uhuru Kenyatta
Baadhi ya viongozi kadha wa kimataifa akiwemo Donald Trump wa Marekani na muungano wa Afrika, AU , walimlaumu Raila wakisema kuwa alikuwa akilielekeza taifa kwa ghasia.
Lakini katika mahojiano kwenye televisheni ya KTN siku ya Alhamisi, Februari 8, Raila alielezea kuwa anaamini kuwa mabalozi hao wanashirikiana na serikali katika kuukandamiza upinzani.
Kulingana na Raila, mabalozi hao wanashirikiana kibiashara na Uhuru Kenyatta na ndio maana wanamuunga mkono na kupuuza kilio cha upinzani.

Habari Nyingine: Muimbaji Jose Chameleon aoyesha mashabiki gari lake jipya la KSh24 milioni
"Mabalozi wa nchi za Magharibi wanaongea kwa manifaa ya nchi zao na wao wenyewe. Wanatumai kupata kandarasi kutoka kwa serikali ya Jubilee na ndio maana wanang'ang'ana sana kuwa katika upande wao," Alisema Raila.
Alijitetea kutokana na utata uliomkabili hasa baada ya kuapishwa akisema kuwa hangeendelea na hatua hiyo kama Jubilee ingeweza kuangazia mwito wao kama upinzani.
Read ENGLISH VERSION
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdia4J3fpZmqZqhnJZ6osDOmmSmmZSWtm65wKmwmmWplri2w8CpmKSZXam8sbGMrp%2BuqqViu6J5zJqZmqSfr7Zuw8BmoqKlkamuqrLAZ5%2BtpZw%3D